Matumizi ya Akiliunde Katika Kutafsiri Matini za Kiutamaduni: Changamoto na Suluhisho

Authors

  • Hadija Jilala

DOI:

https://doi.org/10.61538/huria.v32i2.1928

Abstract

Makala hii inahusu matumizi ya Akiliunde (AI) katika kutafsiri matini za kiutamaduni kwa kuangazia changamoto na suluhisho. Katika kipindi cha sasa cha maendeleo ya sayansi na teknolojia, kumekuwepo na mapinduzi makubwa katika mbinu za kurahisisha kazi mbalimbali za binadamu, ikiwemo kazi ya tafsiri. Miongoni mwa mbinu hizo ni matumizi ya Akiliunde ambayo imekuwa nyenzo maarufu ya kutafsiri matini katika lugha mbalimbali duniani. Hata hivyo, pamoja na ufanisi wake wa kiteknolojia, kuna maswali muhimu yanayojitokeza: Je, Akiliunde inaweza kutafsiri kwa ufanisi matini zenye maudhui ya kiutamaduni? Ni changamoto zipi zinazojitokeza katika matumizi hayo ya Akiliunde? Makala hii imelenga kuchunguza changamato za kutumia Akiliunde kutafsiri matini za kiutamaduni kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Lengo ni kubainisha matini za kiutamaduni, kuchambua changamoto zinazojitokeza katika mchakato wa kutafsiri matini hizo kwa kutumia Akiliunde, na kupendekeza suluhisho la changamoto hizo. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na mbinu ya usaili nusu-funge. Data za makala hii zimewasilishwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli. Nadharia ya Skopos imetumika kama mwongozo wa uchunguzi, uchambuzi na uwasilishaji na mjadala wa data za utafiti huu. Kwa ujumla, makala hii inadhihirisha kuwa ingawa Akiliunde inaweza kurahisisha kazi ya tafsiri, bado inakumbwa na changamoto kubwa katika kufanikisha mawasiliano yenye uzito wa kiutamaduni. Hii ni kwa sababu kila lugha huakisi utamaduni, mitazamo na muktadha wake wa kijamii na kihistoria, ambao si rahisi kutafsiriwa kwa usahihi na mashine bila msaada wa mfasiri binadamu.

Author Biography

Hadija Jilala

The Open University of Tanzania

Downloads

Published

2026-01-09