Kuingiliana kwa Lugha ya Kiswahili na Kiingereza: Uswahilishaji wa Maneno ya Kiingereza

Authors

  • A. Kishe

DOI:

https://doi.org/10.61538/huria.v21i0.47

Abstract

Kuingiliana kwa lugha ni taaluma katika uwanja wa isimu inayohusu lugha zinazoingiliana na kuathiriana. Kuingiliana kwa lugha sio jambo jipya katika dunia. Watu ambao ndio watumiaji wa lugha wamesababisha lugha kuiingiliana waliposafiri au kuhama sehemu moja hadi nyingine kutokana na sababu za kiuchumi, kijamii kiutamaduni na kisiasa. Vilevile lugha huingiliana pale mtu anapotumia lugha mbili au moja baada ya nyingine, kwa maana ya kuchanganya lugha.Historia ya kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili inaonyesha kuwa, lugha ya Kiswahili imeingilina na lugha nyingi. Kwanza kabisa Kiswahili kiliingiliana na lugha ya Kiarabu, katika karne ya 12 wakati Waarabu walipoingia nchini kwa madhumuni ya kuendesha biashara.Baadae ikaingiliana na lugha ya Kijerumani na hatimaye lugha ya Kiingereza katika karne ya 19. Muingiliano wa lugha husababisha muathiriano katika lugha, unaojidhihirisha katika ukopaji wa maneno, athari katika fonolojia, mofolojia sintaksia kwa maana ya mpangilio ya sentensi. Ukopaji wa msamiati ndio athari inayojitokeza zaidi katika lugha zilizoingiliana kuliko athari nyingine yoyote.  Uchanganyaji wa lugha kwa maana ya kubadilisha msimbo ni matokeo ya muingiliano wa lugha. Ili maneno hayo yaweze kuwa sehemu ya lugha ya Kiswahili inabidi yaswahilishwe.  Kuswahilihisha hapa tuna maana ya kuyaingiza maneno yanayokopwa katika muundo wa lugha ya Kiswahili ili yakubalike kuwa sehemu ya msamiati wa lugha hiyo. Mjadala utaonyesha kuwa viwango vya uswahilishaji wa maneno ya Kiswahili si sawa. Makala itahitishimisha kwa kuangalia faida au hasara za kukopa maneno kutoka katika lugha ya  Kiingereza. Makala haya yatajikita katika kujadili muingiliano wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza tu. Data kwa ajili ya makala hii imekusanywa kutoka katika vitabu vinavohusu usanifishaji wa lugha ya Kiswahili, majarida, kamusi, magazeti na nyaraka na taaluma mbalimbali nyingine

Author Biography

A. Kishe

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania  Kitivo cha Sayansi na Sanaa za Jamii, Idara ya Lugha na Fasihi

References

Akida, H. (2008). ―Ukuzaji na Uendelezaji wa Msamiati wa Kiswahili‖ in John G. Kiango (ed) Ukuzaji wa Istlahi za Kiswahili . Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili .Chuo kikuu Dar –es-Salaam, 52-78.

Batibo, H.M. (1996). Loan words clusters nativization rules in Tswana and Swahili: A comparative Study in S. African Journal of African Languagess, 16(2).

Batibo, H.M. (2000). ‗Foreign words as a problem in standardization/lexicography: English and African Loan words in isiXhosa‖ Anja Drame, Department of African Studies, university of Leipzig, Leipzig German, 231-241

Gibbe, A.G (2008) ―Maendeleo ya Istlahi za Kiswahili‖ in John G. Kiango (ed) Ukuzaji wa Istlahi za Kiswahili . Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili .Chuo kikuu Dar –es-Salaam, 79-99.

Karekezi, N. (2007). ―Uundaji wa Istlahi za Kiswahili‖ Makala iliyowasilishwa katika kongamano la kimataifa la Idhaa za Kiswahili Duniani Tarehe 12-15 Oktoba lililoandaliwa na BAKITA.

Massamba, D.P.B (1989:62) ―Development and modernization of Kiswahili Language in Tanzania‖ in F. Coulmas (ed) Language Adaptation. Cambridge, C.U.P, 60-78

Mkude (1986) English in contact with Swahili. In W. Vierreck and W.D Bald

(eds), English in contact With Other Languages Budepest Academia Kiado

Mwansoko, H.J. (1990). ―Swahili modernization in the light of the present language Policy of Tanzania‖. 133-142 in Rubagumya(ed). Langauge

and Education in Africa: A Tanzanian Perspective;

Clevedon/Philadelphia. Multilingual Matters, LTD.

Nurse, D & Spear T (1985). The Swahili: Reconstructing the History and Language of an African Society: University of Pennslavania Press.

TUKI, (1981) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Da-es-Salaam: Oxford University Press.

Thomason, S. & Kaufman, T. (1988). Language Contact creolization and generic Linguitics. Barckley, Calfonia. University of Calfonia Press: 65-109, and 215-28.

Thomason, S. (1976). Contact induced language Changes: loan words and borrowing languages‘s pre- pre borrowing phonology.In Wiiliam Christie, edCurrent Progress in historical Linguitics: Amsterdam: North Holland , 167-179.

Zawawi, S. (1979). Loanwords and their effect on the Classification of Swahili Nominals: Leiden: E. J Brill., 73.

Downloads

Published

2016-02-21